Rafiki yangu mpendwa katika Kristo,
Kila hubiri lina ujumbe ambao unaenda kwa hadhira. Kwa kuwa kiini cha hubiri lolote ni maandiko, ujumbe wako lazima utoke kwenye maandiko. Hivyo, moja ya vitu vya kwanza kufikiria unapoandaa hubiri lako ni fungu au mafungu utakayotumia kwenye hubiri lako.
Lakini pia, badala ya kuanza kufikiria fungu utakalotumia, unaweza kuanza kufikiria mada ya hubiri lako.
Soma : Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuandaa Kichwa Kizuri cha Hubiri Lako
Ukishaamua ni mada gani utatumia, itakuwa rahisi kuamua ni fungu au mafungu yapi utumie. Ili kuamua mafungu au mada ya hubiri, unapaswa kujiuliza maswali kadhaa ambayo yatakuongoza kuamua. Baadhi ya maswali hayo ni haya yafuatayo:
Nini lengo la hubiri lako?
Unapoamua kuhubiri lazima uwe na kitu ambacho umelenga kufanikisha katika hubiri lako. Yaani kabla ya kuamua uhubiri juu ya maada gani, lazima ujiulize: Je, ungependa nini kitokee kwa hadhira yako baada ya hubiri lako?
Ni muhimu kabla ya kuanza kuanda hubiri, uielewe hadhira yako vizuri pamoja na mahitaji yao ili uchague mada inayowagusa. Kumbuka, unahubiri hadhira nzima; siyo mtu mmoja au wachache.
Hivyo, yakupasa kuwa na lengo maalum unapoandaa hubiri na lengo hilo ndilo litakuongoza katika kuchagua fungu au mafungu ya Maandiko au mada. Ruhusu waumini wako wapite mbele ya macho yako ya kiroho ili uweze kujua shida ambazo unaweza kuzungumzia katika hubiri lako. Kwa kifupi, lazima uangalie ukuaji wa kiroho wa hadhira yako aua kanisa lako.
Kipi kinatangulia, kati ya mada na mafungu?
Unaweza kujiuliza, ni kipi unaanza nacho kati ya mafungu ya Biblia utakayo tumia au mada ya hubiri lako. Jibu ni kwamba kwa mahubiri ya kibiblia, unaweza kuchagua mada kabla ya kuchagua fungu lakini si sahihi kuamua utasema nini juu ya mada hiyo kabla ya kusoma fungu.
Ninachommanisha hapa ni kwamba baada ya kuchagua mada, unapaswa kuasoma kwanza mafungu utakayotumia ili uweze kupata kitu cha kusema. Yaani, mafungu ya Biblia ndiyo yakuongoze kusema au yakupatie cha kusema badala ya kuongozwa na mada juu ya nini utasema kwenye hubiri lako.
Soma: Je, Unajua Kuna Aina Ngapi za Mahubiri?
Kama utaamua utasema nini, na baada ya hpo ndipo unachagua fungu litakalo kuwezesha kusema ulichopanga, haya yatakuwa si mahubiri ya kibiblia. Kama nilivyoeleza hapo juu, katika mahubiri ya kibiblia, fungu au mafungu ndiyo hukuongoza useme nini juu ya mada uliyoichagua. Hii hutokea baada ya kusoma fungu au mafungu husika na siyo kabla.
Utatoa aina gani ya hubiri?
Je, hubiri lako ni aina gani kati ya aina tano za mahubiri.
Soma: Je, Unajua Kuna Aina Ngapi za Mahubiri? Soma Hapa
Aina ya hubiri unaloenda kutoa ndiyo itakufanya uamue utumie fungu au mafungu gani na mangapi. Kwa mfano, kama utatoa mahubiri ya kufafanua, mada na maisha ya mashujaa itabidi uchague mafungu zaidi ya mawili. Lakini kama utatoa hubiri la fungu moja au mawili, utachagua mafungu yasiyozidi mawili.
Umesoma nini hivi karibuni?
Mhubiri mzuri ni yule ambayo ni msomaji mzuri wa Neno la Mungu. Kama na wewe unataka kuwa mhubiri mzuri, ni lazima uwe msoamji muzri wa Neno la Mungu. Usipokuwa msomaji mzuri, huwezi kutoa mhaubiri ya kibiblia.
Kama umekuwa katika kujilisha kiroho kwa kusoma Neno la Mungu, ni wazi kuwa utakuwa na mafungu mengi yaliyokugusa. Kama wewe yamekugusa, bila shaka hata wengine yanaweza kuwagusa. Kwa mhubiri, ni vizuri kuwa na taratibu wa kukusanya na kuandika maarifa na visa unavyokutana navyo kila unapojifunza Biblia. Hivi vinaweza kukusaidia baadaye kuandaa mahubiri na kufanya kazi yako ya kuandaa mahubiri kuwa rahisi.
Zaidi ya kuchagua mada na mafungu ya kutumia katika hubir lako, kitu kingine muhimu ni kichwa cha hubiri. Kwa kawaida, kichwa cha hubiri kinaandaliwa mwisho baada ya kuwa umeshapata mada na mafungu na umeshaamua utasema nini juu ya mada na mafungu yako.
Zingatia haya ili uweze kuanda hubiri lenye ujumbe muafaka kwa hadhira na tukio husika.
Je, Ungependa Kujifunza Zaidi Kuhusu Mada hii?
Kama unataka kujifunza kwa kina kuhusu mada hii na mambo mengine kuhusu namna ya kuandaa na kuwasilisha mahubiri yenye mvuto kwa hadhira, unaweza kujipatia kitabu kizuri kiitwacho Homilia kwa Walei: Ustadi wa Kuandaa na Kuwasilisha Mahubiri.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa namna ambayo ni rahisi kueleweka kwa kila mtu kikimlenga hasa yule asiye na elimu ya Teolojia. Kitabu hiki kinawafaa watu wote wanaohubiri Neno la Mungu katika maeneo mbalimbali kama vile katika ibada ya kawaida kanisani, ibada maalum za kanisani kama vile ibada ya maombi katikati ya juma, mikutano ya uamsho na majuma ya maombi, mahubiri ya hadhara na matukio mengine ambapo mahubiri hutolewa.
Ili kupata kitabu hiki, wasiliana nasi kupitia namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (Devotha Shimbe) na Email: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com.
Je, unataka kupata mafunzo endelevu kuhusu mafaniko kwa mkristo?
Kama unataka kuendelea kujifunza kuhusu masuala mbalimbali juu ya mafanikio kwa mkristo unaweza kujiunga na mtandao huu ili uweze kupata makala mbalimbali. Kwa kufanya hivyo, utapata makala kupitia email yako kila zinapowekwa katika mtandao huu.
Ili kujiunga, jaza fomu iliyoko hapa chini.