Rafiki yangu mpendwa katika Kristo,
“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu” (Waebrania 13:4). Haya ni maelekezo ya Mungu yenye lengo la kuwafanya wanandoa wasifanye tendo la ndoa na mtu mwingine asiye mwenzi wao wa ndoa. Hata hivyo, hali halisi haiku hivyo, baadhi ya wanandoa, si waaminifu katika ndoa ndoa zao, wanafanya tendo la ndoa na watu wengine, yaani wanachepuka.
Katika tamaduni nyingi, ni kitu cha kawaida mwanaume kutoka nje ya ndoa na wakati mwingine kuwa na mke zaidi ya mmoja aliye halali au hata siye halali kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za jamii yake. Katika mazingira haya, inaonekana kuwa wanaume ndio wanatoka nje ya ndoa zaidi kuliko wanaume. Hata hivyo, tafiti za hivi karibuni, hasa katika nyingi zilizoendelea, zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa wanaongezeka na wanakaribia kuwa sawa na wanaume.
Mfano wa tafiti kuhusu hali ya uaminifu katika ndoa ni ni utafiti uliofanywa na taasisi ya Kinsey ya Indiana,Marekani. Katika utafiti huo, katika wanandoa wenye wa umri wa miaka 3, hakukuwa na tofauti kubwa ya uaminifu katika ndoa kwa wanaume na wanawake (asilimia 23 ya wanaume walikuwa na mahusiano nje ya ndoa wakati wanawake wenye mahusiano nje ya ndoa walikuwa 19%).
Utafiti mwingine ni ule uliofanywa na Kituo cha kukusanya maoni cha taifa (National Opinions Research Centre) cha Marekani uliofanyika mwaka 2018 ambao ulibaini kuwa wanawake wenye umri wa miaka kati ya 18 na 29 walikuwa na uwezekano mkubwa kidogo wa kutoka nje ya ndoa kuliko wanaume wenye umri huo, yaani asilimia 11 ya wanawake na asilimia 10 ya wanaume walitoka nje ya ndoa). Takwimu zaidi za taasisi hiyo zinaonesha kuwa wanawake wanaotoka nje ya ndoa waliongezeka kwa asilimia 40 kwa kipindi cha kati ya mwaka 1990 na 2010 wakati idadi ya wanaume iliongezeka kwa asilimia 21 tu.
Bahati mbaya, katika nchi zinazoendelea, hakuna takwimu za uhakika kuhusu suala hili, lakini hali inaweza iswe tofauti. Hata kama hakuna takwimu katika nchi zetu, lakini ukweli ni kwamba wanawake na wanaume wana michepuko. Inashangaza kwamba hata wanandoa wanaoonekana kuwa wanapendana, baadhi yao wana michepuko. Cha kushangaza zaidi, hata wakristo wanaompenda Mungu nao wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kuchepuka.
Sijui kama umewahi kujiuliza kwanini wanandoa hutoka nje ya ndoa? Zipo sababu nyingi zinazowafanya wanandoa kutoka nje ya ndoa. Zipo sababu za jumla na zipo sababu za wanaume na pia zipo sababu za wanawake tu. Leo tutaangalia kwa ni wanawake huchepuka? Tutaangalia sababu zilizobainishwa na tafiti mbalimbali pamoja na wataalam wa masuala ya mahusiano.
Baadhi ya sababu za wanawake kuchepuka ni hizi zifuatazo:
Kutokuridhishwa na mahusiano
Sababu mojawapo inayowafanya wanawake kuchepuka ni kutokuridhika na mahusiano waliyomo. Kwa mfano, mwanaume anaweza kuwa hamjali mwanamke kiasi cha kujisikia kana kwamba hajaolewa. Katika mazingira haya, akitokea mwanaume anayeonesha kumjali sana mwanamke huyo ni rahisi kumwangusha. Kumjali mwanamke haimanishi kumpatia pesa nyingi au kumpatia mahitaji yake yote. Haya ni muhimu lakini kuna zaidi ya hapo. Hata kuwa karibu naye tu kama vile kumpa company na kumpatia faraja anapokuwa na changamoto ya aina yoyote iwe ndogo aua kubwa kunaweza kumridhdisha mwanamke zaidi hata ya kumpatia fedha nyingi.
- Kujiona duni
Mwanamke anapokuwa anajiona duni (low self-esteem) na ikatokea mume wake hawezi kumfanya ajione wa maana anaweza kujikuta anatafuta vyanzo vya kufunika hali hiyo. Anapotokea mtu anayeonesha kuwa amevutiwa na mwanamke huyo, ni rahisi kwa mwanamke huyo kuvutwa kwa mwanaume huyo. Ili kumfanya mwanamke asitafute mtu wa kumfanya ajisikie wa maana na asiye duni, yapasa mume wake amtengenezee mazingira ya kujisikia wa maana na muhimu sana. Zipo njia nyingi za kumfanya mke ajisikie wa maana. Njia moja wapo ni maneno. Wewe mwanaume, jitahidi kumwambia mke wako maneno ya kumfanya ajisikie wa maana kama vile kumpongeza au kumsifia anapofanya jambo vizuri, kueleza namna alivyo mzuri na anavyokuvutia, kuepuka kusema maneno hasi dhidi yake na kujiepusha kumkosoa kupita kiasi.
- Njaa ya kihisia
Wakati tafiti zinaonesha kuwa, wanaume huchepuka ili kutosheleza tamaa za kimwili, kwa upande wa wanawake, hii siyo sababu kubwa kwao. Sababu mojawapo inayowafanya wanawake kuchepuka ni kutosheleza mahitaji ya kihisia. Wanawake ni viumbe wa kihisia (emotional being) kwa maana ya kwamba wanafanya mambo mengi kwa kusukumwa na hisia na wasipotoshelezwa kihisia na waume zao watatafuta kutoshelezwa nje ya ndoa. Baadhi ya vitu vinavyowatosheleza kihisia ni mazungumzo mazuri na chanya, kuonewa huruma, kuheshimiwa, kupendwa, kuungwa mkono katika mambo yao na kadhalika. Ikitokea mume hawezi kukaa na kuongea na mke wake vizuri, haoneshi upendo wa dhati kwa maneno na vitendo, hamuungi mkono katika mambo yake, haoneshi huruma na kujali, haoneshi kujitoa katika mambo ya mke wake na kadhalika, kuna uwezekano mwanamke akatoka nje ya ndoa ili kutafuta kutimimiziwa mahitaji haya.
- Njaa ya tendo la ndoa
Pamoja na kwamba tendo la ndoa siyo sababu kubwa ya kuchepuka kwa wanawake, kuna mazingira ambapo wanawake wasipotoshelezwa katika tendo la ndoa wanaweza kuchepuka. Kwa mfano, wapo baadhi ya wanawake ambao huwa hawafiki kileleni wakati wa tendo la ndoa kiasi kwamba kila wanapofanya tendo hilo hubaki njaa. Hii ni kwa sababu raha ya tendo la ndoa hutokea pale mtu anapofika kileleni. Sasa, mwanamke asipofika kileleni, anaweza kutamani kuchepuka ili akapate traha hiyo anayokikosa.
Kama wewe ni mwanaume na unataka mke wako asichepuke, huna budi kujifunza mbinu mbalimbali za kumtosheleza mke wake katika tendo la ndoa ikiwa pamoja na kumfikisha kieleleni ali asibaki na njaa ya tendo la ndoa.
- Upweke
Kama ambavyo tumeshaona hapo juu, mwanamke ni mtu wa hisia na anajisikia vizuri pale ambapo mume wake anakuwa karibu naye. Yapo mazingira yanayoweza kumfanya mwanamke asiwe karibu na mume wake. Kwa mfano, mume anaweza kuwa anaishi sehemu nyingine kwa sababu za kikazi, mume kuwa na shughuli nyingi kiasi cha kuosa muda na mke wake, au wote wawili kuwa na shughuli nyingi. Ili kuepusha hali hii isitokee, yafaa wanandoa kutengeza mazingira ya aina yoyote yatakayomuondolea mwanamke upweke ili asije akachepuka.
Ungependa kujifunza zaidi kuhusu mada hii ?
Nikusihi uendelee kufuatilia mtandao huu ili tuweze kujifunza kuhusu mada hii. Mtandao umesheheni makala nzuri kuhusu masuala mbalimbali kama vile mahusiano (uchumba na ndoa), malezi ya watoto, fedha, biashara na uwekezaji.
Ili usiptwe na chchote, unaweza kujiunga na mtandao huu ili uweze kupata makala hizo moja kwa kwa moja kwenye email yako kila zinapowekwa mtandaoni.
Ili uweze kujiunga, jaza fomu iliyoko hapa chini.