Rafiki yangu mpendwa, Leo ni siku muhimu kwa Watanzania—Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Wananchi wanachagua viongozi wa vijiji, mitaa, na vitongoji, wakiwemo wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa. Kama viongozi mbalimbali walivyosisitiza, uchaguzi huu una umuhimu mkubwa kwa maendeleo yetu. Kwa hiyo, tunapaswa kujitokeza kwa wingi na kutumia haki yetu ya kikatiba kuwachagua viongozi…