Haya ndiyo mambo muhimu ya kuzingatia katika uwekezaji

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo,

Watu wengi hutamani kuingia katika uwekezaji ili wawe na kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Kwa upande mwingine, kuna watu wengi ambao hawataki kuingi katika uwekezaji kwa kuogopa hatari zilizoko kwenye uwekezaji. Vilevile, kuna wawekezaji ambao huamua kuondoka kabisa katika uwekezaji na kufanya shughuli zingine baada ya kukumbana na changamoto au hatari za uwekezaji na wakashindwa kunufaika na uwekezaji wao.

Yapo mambo muhimu ambaye kila anayetamni kuingi katika uwekezaji au aliye tayari katika uwekezaji wa aina yoyote anapaswa kuyafahamu na kuyazingatia ili aweze kufanikiwa. Mambo hayo yasipozingatiwa, uwekezaji unaweza usifanikiwe.

Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatavyo:

  1. Wekeza zaidi kwenye rasmali zinazoingiza fedha kuliko zinazotoa fedha

 Lengo la uwekezaji wowote ni kuingiza fedha na siyo kutoa fedha. Uwekezaji unaweza kufanyika kupitia raslimali unazomiliki. Kuna aina mbili za raslimali ambazo watu wanamiliki. Aina ya kwanza ni raslimali zinazoingiza fedha au faida (assets) na aina ya pili ni raslimali zinazotoa fedha mfukoni mwako (liabilities). Kwa bahati mbaya, watu wengi wanachanganya kati ya assets na liabilities wakidhani kuwa wana miliki assets kumbe walichonacho ni liabilities. Mfano wa assets ni kama vile ardhi, nyumba ya kupangisha, magari ya biashara na kadhalika. Mifano ya liabilities ni nyumba ya kuishi, gari la kutembelea, televisheni na kadhalika.

Unachopaswa kufahamu ni kwamba ili kufikia mafanikio ya kifedha, unapaswa kuwa na assets nyingi kuliko liabilities ili uweze kuingiza fedha nyingi zaidi kuliko unazotoa. Lakini ukiwa na liabilities nyingi zaidi kuliko assets unaweza kuwa unatoa fedha nyingi zaidi kuliko unazoingiza na kwa mazingira hayo inaweza kuwa vigumu kwako kufikia mafanikio ya kifedha.

2. Uwekezaji una hatari zake.

 Unapowekeza usijipe asilimia 100 kuwa utapata faida badala yake tambua kuwa kuna uwezekano wa kupoteza kile ulichowekeza. Hivyo, unatakiwa kuwa makini sana kabla ya kuwekeza. Hata hivyo, hata kama utakuwa makini kiasi gani, bado huwezi kujihakikishia kuwa utapata faida. Kwa sababu hiyo, unapowekeza, uwe tayari kwa lolote. Na ikitokea umewekeza halafu, kwa sababu moja ama nyingine, ukapoteza, basi usikate tamaa badala yake chukulia kupoteza huko kama somo litakalokuwezesha kufanya vizuri zaidi utakapowekeza tena.

3. Usiwekeze kwenye kitu usichokijua

George Classon, katika kitabu chake “The Richest man in Babylon” anashauri kuwa mtu asiwekeze katika eneo ambalo halifahamu vizuri. Kwa mujibu wa Classon, fedha hung’ang’ania kwenye ulinzi wa mmiliki mwenye tahadhari ambaye huwekeza chini ya ushauri wa watu wenye hekima juu ya uwekezaji wake. Watu wenye hekima ni watu wenye ufahamu kuhusiana na uwekezaji ambao unaufanya.

Pamoja na kupata ushauri kutoka kwa watu wenye hekima, wewe mwenyewe unapaswai uchukue muda kujifunza juu ya uwekezaji unaotaka kuufanya ili uwe na uhakika na kile unachokifanya kwa ajili ya usalama wa fedha yako. Classon anaelezea pia kuwa fedha humpotea yoyote ambaye huwekeza kwenye eneo ambalo hana uelewa juu yake au eneo ambalo halijathibitishwa na wale ambao wana ujuzi juu yake. Kwa maneno maneno, mwekezaji makini haingii “kichwa kichwa” kwenye uwekezaji.

Biblia inasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” (Hosea 4:9). Unaweza kuangamia katika uwekezaji kwa kukosa maarifa ya uwekezaji. Hivyo, ni vema utafute maarifa ya kutosha kuhusu uwekezaji wako kabla ya kuanza kuwekeza na uendelee kujiongezea maarifa kila siku. Kwa kufanya hivyo, utaweza kujua uwekezaji wako na kuepuka uwekekano wa kuangamia. Usikubali kuangamizwa kiuwekezaji kwa kukosa maarifa.

4. Usiweke mayai yote kwenye kapu moja

Kutoweka mayai kwenye kapu moja maana yake ni kutawanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali badala ya kuwekeza kwenye eneo moja tu hata kama lina faida kubwa. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuepuka hasara kama uwekezaji huo hautafanya vizuri. Hii ni kutokana na ukweli kwamba uwekezaji una hatari zake na hivyo lolote linaweza kutokea.

Je, unapenda kujifunza zaidi kuhusu masuala ya uwekezaji?

Basi jipatie kitabu chetu kiitwacho “Siri za Mafanikio ya Kifedha kwa Mkristo: Elimu ya Fedha isiyofundishwa Shuleni. Katika kitabu hiki utapata maarifa ya msingi kuhusu nasuala mablimbali kama vile uwekezaji, biashara, kazi, nidhamu ya fedha , dhana ya utajiri kwa mkristo na mengine mengi.

Wasiliana nasi ili kupata kitabu hicho kwa kupitia namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (Devotha Shimbe) na E-mail: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com.

Vilevile, kama unahitaji kupata maarifa kuhusu mafanikio katika maeneo mengine, unaweza kujiunga na mtandao huu kwa kubofya hapa ili uweze kupata makala moja kwa moja kupitia email yako.  Mtandao huu umeanzishwa kwa kusudi la kuwapatia maarifa ya msingi katika nyanja mbalimbali za maisha. Katika mtandao huu utapata maarifa katika maeneo ya fedha, biashara, uwekezaji, mahusiano, malezi ya watoto na mambo ya kiroho.

About Simeon Shimbe

Simeon Shimbe ni mchumi kitaaluma, mwandishi wa vitabu na makala na mjasiriamali. Amekuwa akiandika kuhusu masuala ya fedha, biashara na uwekezaji na masuala mbalimbali ya kiroho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *