Rafiki yangu mpendwa katika Kristo,
Katika dunia ya leo, karibu kila mtu analalamika juu ya ugumu wa maisha. Hata wafanyakazi wenye ajira za kudumu nao ni miongoni mwa watu wanaolalmikia ugumu wa maisha.Watu wanapata pesa kila siku au kila mwezi lakini watakuambia haitoshi. Umewahi kujiuliza tatizo ni nini? Zinaweza kuwepo sababu nyingi kwa nini karibu kila mtu analalamikia ugumu wa maisha, lakini sababu mojawapo ni kwamba watu wengi wanachanzo kimoja tu cha kipato. Kwa mfano, unaweza kuwa umeajiriwa na una kipato kikubwa lakini kama haunanchanzo kingine cha kipato, utaendelea kulalamika hadi siku unastaafu na ukistaafu maisha yatakuwa magumu zaidi. Huo ndio ukweli.
Kutokana na ukweli huu, kama unataka kujikwamua na changamoto za kifedha zinazokusababishai ugumu wa maisha, ni muhimu kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Chanzo kimojawapo cha kipato ni biashara. Biashara ni shughuli yoyote inayohusisha ubadilishanaji wa bidhaa na huduma kwa ajili ya kupata faida. Mara nyingi katika biashara, pesa hutumika kama njia ya ubadilishanaji wa bidhaa au huduma. Katika muktadha huu, hata mtu aliyejiajiri anahesabika kama ni mtu anayemiliki biashara maana ajira binafsi kwa vyovyote vile huhusisha mabadilishano ya bidhaa au huduma.
Kwa nini ni muhimu kuwa na biashara?
Ndugu yangu mpendwa, pamoja na vyanzo vingine vya kipato unavyoweza kuwa navyo, ni muhimu pia kuwa na biashara. Biashara ni njia mojawapo ambayo inaweza kukupatia kipato kisicho na kikomo.Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba biashara inaweza kutupatia kipato kisicho na kikomo, lakini watu wengi wanaogopa kuingia katika biashara kutokana na sababu mbaimbali. Pamoja na sababu yoyote unayoweza kuwa nayo ya kutokuwa na biashara, haiwezi kuondoa umuhimu wa biashara. Mtu yeyote aliyedhamiria kutafua mafanikoo ya kifedha ni muhimu kuwa biashara.
Kwa nini ni muhimu kila mtu kuwa na biashara?
Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwa nini ni muhimu kila mtu awe na biashara:
Biashara huleta kipato kisicho na ukomo
Kama nilivyodokeza awali, biashara ni njia ya uhakika ya kupata kipato kisicho na kikomo ukilinganisha na kazi ya kuajiriwa na kujiajiri. Hakuna mtu anayekupangia ukomo wa kipato chako katika biashara. Kinachoamua upate kipato kiasi gani ni juhudi na maarifa yako. Hata kama ikitokea biashara moja ikafikia ukomo, unaweza kuanzisha biashara nyingine au kupanua iliyopo.
Biashara ni urithi wa watoto wako na vizazi vyako
Mojawapo ya vitu vinavyoaminika kuwa ni urithi kwa watoto ni elimu. Dhana hii ipo siku nyingi kuwa sana katika jamii zetu nyingi nab ado inaaminika hivyo hata leo. Ni kweli kabisa , elimu bado ni muhimu lakini dhana hii umepitwa na wakati kwa sasa. Mtoto anaweza akapata elimu nzuri na ya gharama kubwa lakini ikumbukwe kuwa mfumo wetu wa elimu unamwaandaa mtoto kuwa mwajiriwa tu. Na kwa kuwa nafasi za ajira ni changamoto siku hizi na hata akibahatika kupata ajira bado kipato cha ajira hakiwezi kumpatia uhuru wa kifedha. Hivyo, urithi unaoweza kumfaa mtoto wako leo, siyo elimu bali ni biashara. Kama wewe ni mwajiriwa na una mtoto aliyesomea fani yako bado hawezi kurithi kazi yako. Hata kama mzazi una kazi nzuri na inayokulipa vizuri, siku ukifariki au ukistaafu ndiyo mwisho wa kazi yako, mtoto wako hawezi kuchukua kazi hiyo. Lakini ukiwa na biashara na ikatokea ukastaafu au kufariki dunia, mtoto wako anaweza kurithi biashara hiyo na akaindeleza na yeye akifariki, watoto wake watairithi na kuiendeleza pia. Kama biashara itaendeshwa vizuri na ikaendelea kuwepo, inaweza kurithishwa kwa vizazi vingi vya baadaye.
Kwa kuwa ni mpango wa Mungu kuwa tufanikiwe katika mambo yote (3 Yohana 2:) ni vizuri tutafute njia za kujipatia kipato zitakotuwezesha kufanikiwa kifedha. Njia moja wapo ya kufikia mafanikio ya kifedha ni biashara. Biblia inaonesha kuwa biashara inaleta utajiri, inatuwezesha kupata mahitaji yetu muhimu na hata Mungu mwenyewe aliwahimiza watu wake wafanye biashara kama mafungu yafuatayo yanavyoonesha:
Biashara huleta mali
“Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo” (Mwanzo 34:10).
Biashara hutupatia mahitaji yetu muhimu
“Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari’’ (Isaya 23:18).
Biashara huleta utajiri
“Kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako” (Ezekieli 28:5).
Je, unataka kujifunza zaidi kuhusu mafanikio?
Basi jipatie kitabu chetu kinachoitwa Siri za Mafanikio ya kifedha kwa Mkristo: Elimu isiyofundishwa Shuleni. Ili kupata kitabu hiki, wasiliana nasi kupitia namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (Devotha Shimbe) na E-mail: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com.
Je, unataka kupata mafunzo endelevu kuhusu mafanikio kwa mkristo?
Kama unataka kuendelea kujifunza kuhusu masuala mbalimbali juu ya mafanikio kwa mkristo unaweza kujiunga na mtandao huu ili uweze kupata makala mbalimbali. Kwa kufanya hivyo, utapata makala kupitia email yako kila zinapowekwa katika mtandao huu.
Ili kujiunga na matandao huu, jaza fomu iliyopo hapa chini.