Mtandao huu umejikita katika kutoa elimu kwa watu wote ambao wamechagua kufanikiwa katika mambo yote, yaani kiuchumi, kiroho na kimahusiano.
Tofauti na wengine, sisi tunayaangalia mafanikio katika mapana yake yote na si eneo moja tu la kiuchumi kwa maana Neno la Mungu linasema “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo (3 Yohana 1:2).
Kufanikiwa kiuchumi tu hakutoshi. Unaweza kuwa na mafanikio kiuchumi lakini usiwe na mahusiano na watu (familia yako na jamii).
Unaweza kuwa na mafanikio kiuchumi lakini ukawa na afya mbaya kiasi kwamba ukashindwa hata kufaidi fedha uliyo nayo. Lakini pia unaweza kufanikiwa kiuchumi lakini ukaishi maisha yasiyompendeza Mungu na ukakosa nafasi katika uzima wa milele.
Hivyo, kwetu sisi mafanikio ni kufanikiwa katika mambo yote ikiwa pamoja na kiuchumi, kiafya, kimahusiano na kiroho. Hivyo, huduma zetu zinalenga kumsaidia mtu kufanikiwa katika maeneo yote hayo.
HUDUMA ZETU
- Makala za mafunzo
Kupitia mtandao huu utapata makala zenye mafunzo na hamasa ya kupiga hatua zaidi ili kuweza kufanikiwa katika mambo yote yakiwemo maeneo ya fedha, biashara, uwekezaji, mahusiano, malezi ya watoto na mambo mengine ya kiroho.
- Kutoa makala na mafunzo kwa njia ya email
Zaidi ya kuweka makala zetu kwenye mtandao huu, pia tunatuma BURE makala hizi moja kwa moja kwa mtu yeyote anayehitaji. Ili uweze kupokea makala hizo bonyeza maandishi haya.
- Vitabu vya mafanikio
Tumeandika vitabu kadhaa kuhusiana na maeneo mbalimbali ya mafanikio. Vitabu hivyo vipo katika mfumo wa nakala ngumu (hard copy) na nakala laini (soft copy). Tunavyo vitabu vizuri kuhusu Elimu ya fedha, Mahusiano (Uchumba na Ndoa), Malezi ya watoto Mwonekano wa Mkrisito (mapambo,.mavazi na vipodozi) na masuala mengine ya kiroho. Unaweza kuvipata kwa kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano yaliyoko chini ya maelezo haya.
- Ushauri wa moja kwa moja
Tunatoa ushauri kuhusu masuala ya fedha, biashara, uwekezaji, mahusiano, malezi ya watoto na masula amengine ya kiroho. Unaweza kuwasiliana nasi na kupata ushauri kuhusu mafanikio katika maeneo hayo.
- Mafunzo ya ana kwa ana
Tunatoa mafunzo maalum kwa watu wanaotualika kulingana na mahitaji yao. Mafunzo haya tuyatoa kwa watu katika makundi kama vile makanisa, jumuia za kidini mashuleni na vyuoni, vikundi vya wafanyabiashara kama vile mama ntilie, wamachaninga, bodaboda,wananchama wa SACCOS na VICOBA na makundi mengine. Mafunzo haya yatakuwa ya ana kwa ana lakini yanaweza kutolewa kwa njia ya mtandao pale inapobidi.
- Kundi maalum la mafunzo
Tunatoa mafunzo katika kundi maalum la wasapu kwa wale wanaotaka kupata mafunzo endelevu.Mafunzo haya yanalipiwa.
MAWASILIANO YETU
Unaweza kuwasiliana nasi kuhusu jambo lolote kwa kutumia nia zifuatazo:
Namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (DevothaShimbe)
EMAIL: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com