Rafiki yangu mpendwa Katika Kristo, Neno la Mungu linaeleza kuwa “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. Akawakumbatia,…
All posts by Devotha Shimbe
About Devotha Shimbe
Devotha Shimbe ni Mwalimu na mwanasaikolojia. Amepata pia mafunzo ya Theolojia. Devotha amejitoa kumtumikia Mungu katika maisha yake yote na amekuwa akifundisha na kutoa semina mbalimbali kuhusu mahusiano na maisha ya kiroho kwa ujumla.
Hivi ndivyo Akina Mama wanavyoweza kuwapeleka Watoto kwa Yesu
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Katika malezi ya watoto kikristo, wazazi wote wawili wana nafasi yake. Japo wanatakiwa kushirkiana lakini baba ana nafasi yake mahususi na mama pia ana nafasi yake. Tayari tumeshaona kwa kifupi namna gani akina baba wana walivyo na mchango katika kumpeleka mtot kwa Yesu. Katika makala ya leo tutaangalia mchango wa…
Hivi ndivyo akina baba wanavyoweza kuwapeleka watoto wao kwa Yesu
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Mwalimu mmoja asiyeamini kwamba Mungu yupo (atheist), siku moja alimtuma mwanafunzi wake kwenda nje ya darasa na kungalia juu. Aliporudi mwalimu aliuliza, umeliona anga? Umeyaona mawingu? Umeuona mwanga wa jua? Mwanafunzi alikuwa akijibu “ndiyo” kwa kila swali. Na mwisho mwalimu alimuuliza, “Umemuona Mungu”? Mwanafunzi alijibu “Hapana”. Kufuatia jibu hilo mwalimu…
Hivi Ndivyo Mnavyoweza kusimamia Fedha katika Ndoa Yenu
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Mtu mmoja aliwahi kusema “kila ndoa ina rangi yake” akiwa na maana kuwa ndoa hazifanani katika namna wanandoa wanavyoendesha mambo yao. Moja ya mambo ambayo kuna tofauti kubwa kati ya ndoa moja na nyingine ni namna wanandoa wanavyosimamia pesa zao. Kuna aina mbalimbali za wanandoa kuhusiana na namna wanavyosimamia masuala…
Mavazi ya kujisitiri yanayotajwa na Biblia ni yapi?
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Suala la mavazi yanayomfaa mkristo ni mojawapo ya masuala tete katika ulimwenguni wa leo wenye mwingiliano wa tamaduni mbalimbali unaosabishwa na utandawazi. Kwa miaka ya nyumba hakukuwa na kelele nyingi sana kuhusu suala hili maana watu wengi walikuwa wanavaa mavazi ya kujisitiri. Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali, watu wanaiga…
Fedha yako inaweza kuimarisha au kubomoa Ndoa yako
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Tafiti zilizofanyika katika nchi mbalimbali zinaonesha kuwa mojawapo ya mambo yanayooongoza kusababisha migogoro na kuvunjika kwa ndoa ni fedha. Kwa mfano, Mwaka 2017, kampuni moja ya kimarekani inayojishughulisha na utafiti na utoaji wa elimu ya masuala ya fedha itwayo Ramsey solutions, ilifanya utafiti uliowahusisha watu 1072 nchini humo. Lengo la…
Je, Mungu anajali unavyovaa na kujipamba?
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Baadhi ya watu hudhani kuwa namna mtu anavyoonekana kwa watu wengine si muhimu ili mradi tu ndani ya moyo wake yuko safi wakidai kuwa Mungu haangalii nje bali anaangalia ndani ya moyo tu. Je, ni kweli Mungu anaangalia muonekano wa ndani pekee na hajali kabisa mwonekano wa nje? Ni kweli…
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kufundisha na Kuhubiri Kwa Watoto wa Siku Hizi
Rafiki yangu mpendwa katika Krsito, Tunaishi katika karne ambayo imepewa jina la “Karne ya Sayansi na Teknolojia”. Maendeleo makubwa ya Sayansi na teknolojia yamesababisha mabadiliko karibu katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu na mabadiliko hayo yanatokea kwa kasi sana kuliko karne zilizopita. Maendeleo tunayoyashuhudia si kitu cha kushangaza kwa wasomaji wa Biblia maana ni…
Unajua Umuhimu wa kuwafundisha watoto elimu ya kiroho?
Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wana wasiwasi kuhusu kuwalea watoto katika ulimwengu wa leo unaokabiliwa na changamoto za utandawazi. Hata hivyo, hatuna sababu ya kuwa na wasiwasi kama tukifuata ushauri huu: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee”(Mithali 22:6). Watoto waendeleapo kukua, wanahitaji ‘njia’, yaani kanuni…
Hiki Ndicho Mungu Aliagiza Tufanye Kabla Ya ‘Kula Bata’
Rafiki yangu mpendwa, Katika makala yangu iliyopita, nilieleza vile namna ambavyo Mungu aliagiza “tule bata”. Katika makala hiyo nilieleza kuwa kula bata kunatafsiriwa kama kupumzika na kufurahia maisha. Kupitia biblia, Mungu ameelekeza tuwe na muda kupumzika vya kutosha kila siku na siku moja kwa kila juma. Leo nitakushirikisha kitu muhimu cha kuzingatia kabla ya “kula…