Ukifanya Haya Utajiepusha na Hatari ya Kuingia Kwenye Madeni Mabaya

Rafiki yangu mpendwa, Karibu tena katika mwendelezo wa makala kuhusu mikopo na madeni. Katika makala ya nyuma nimekuwa nikikushirikisha mambo kadhaa kuhusu mada hii. Pamoja na mambo mengine, tumejifunza kuwa hakuna andiko lolote katika Biblia linalosema kwamba kukopa ni dhambi au kukopesha ni dhambi na kwamba yapo mafungu kadhaa ambayo ama moja kwa moja au…

Unahitaji Kujua Kweli Hizi Kabla ya Kuchukua Mkopo Wowote

Rafiki yangu Mpendwa, Suala la madeni yatokanayo na mikopo linawatesa wengi. Sababu mojawapo ya hali hii ni kwamba kuna kweli nyingi ambazo watu hawazijui kuhusu mikopo na pia kuna upotoshaji mwingi sana kuhusu mikopo. Kwa mfano: Fuatana nami nami  katika makala haya ninapoangazia hoja hizi: Kigezo cha kuzingatia unapochukua mkopo ni kimoja tu Ikitokea unahitaji…

Kama Unataka Usiteseka na Madeni, Fahamu Tofauti Kati ya Mikopo Mizuri na Mikopo Mibaya

Rafiki yangu Mpendwa, Pamoja na ukweli kwamba watu wengi wanateswa na madeni yatokanayo na mikopo lakini wapo watu ambao mikopo imewaleta mafanikio makubwa. Sasa unaweza kujiuliza, kwa nini baadhi ya watu wanufaike na mikopo wakati wengine iwatese? Sababu ya tofauti hii iko katika aina ya mkopo ambao mtu anauchukua. Mikopo inayowatesa watu wengi ni mikopo…

Hizi Ndizo Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuogopa Madeni Kama Ukoma

Rafiki yangu mpendwa, Mwandishi maarufu wa karne ya 19 na 20 wa vitabu vya kikristo na machapisho mengine aitwaye Ellen G. White, katika kitabu chake kiitwacho Counsels on Stewardship, uk. 272 ameandika “Ni lazima kuwepo na zingatio makini kuhusu uchumi, la sivyo deni kubwa litapatikana. Dumu katika mipaka. Epuka upatikanaji wa deni kama vile ambavyo…

Biblia Inasemaje Kuhusu Kukopesha kwa Riba?

Rafiki yangu mpendwa, Katika makala yaliyopita, tuligusia kidogo suala la kukopesha kwa riba. Katika makala ya leo, tutaliangalia suala hili kwa undani kidogo ili kuona kama Biblia inaruhusu kukopesha kwa riba au ala. Kusoma makala juu ya ‘Biblia inasemaje kuhusu kukopa na kukopesha’ bonyeza hapa Biblia imetoa miongozo bayana kuhusu kukopeshana ambapo imeeleza ni nani…

Biblia Inasemaje Kuhusu Kukopa na Kukopesha?

Rafiki yangu Mpendwa, Mikopo na madeni ni sehemu ya maisha kwa watu wengi leo. Pamoja na manufaa makubwa yanayoweza kupatikana kupitia mikopo, kuna changamoto na hatari nyingi zinazotokana na mikopo. Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye madeni mabaya na yanayowatesa kwa sababu tu hawajui hatari za mikopo, na hilo limekuwa kikwazo kikubwa kufikia mafanikio ya kifedha.…

Mtu Makini Kama Wewe Hupaswi Kushiriki Michezo ya Bahati Nasibu

Rafiki yangu mpendwa, Mimi siyo mfuatiliaji kabisa wa vyombo vya habari. Lakini siku ya leo nimejikuta nasikiliza matangazo ya kituo kimoja cha radio wakati napata chakula katika mgahawa fulani. Kila baada ya muda kulikuwa na matangazo ya biashara yanayohamasisha wasikilizaji kubeti ili kubashiri matokeo ya mechi za mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea huko Qatar.…

Kama Unadhani Kuwasaidia Omba Omba Ndiyo Ukristo, Soma Vizuri Biblia Yako

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Mojawapo ya changamoto ambayo inaelekea kuwa janga hapa nchini na duniani kwa ujumla ni omba omba. Ninapozungumzia ombaomba simaanishi wale tu wanaosimama au kutembea mitaani na vibakuli kuomba misaada. Ndiyo, hao ni omba omba, lakini pia wapo omba omba wasiotembea au kusimama mitani lakini wanaomba misaada kwa njia mbalimbali. Baadhi…

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukwepa Gharama za Miamala ya Fedha ya Kielektroniki bila Kuvunja Sheria

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Kutokana na maendeleo ya Sayansi na teknolojia yaliyopo, siku hizi utunzaji na uhamishaji wa fedha umekuwa rahisi sana. Unaweza kutunza fedha kwa namna nyingi kama vile kwenye akaunti ya benki na kwenye simu za mikononi kupitia akaunti ya M-pesa, Tigo-Pesa, Airtel Money, Halopesa, Esy-Pesa na T-Pesa. Siku hizi unaweza kuhamisha…

Kwa Nini Watu Wengi Wanapenda Kuajiriwa Licha ya Ajira Kutowapatia Mafanikio ya Kifedha?

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Wafanyakazi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado wanasikilizia maumivu baada ya kupata pigo kubwa mwezi huu. Pigo hilo ni nyongeza ndogo ya mshahara isiyolingana na matarajio yao na isiyolingana na hali halisi ya ugumu wa maisha uliopo. Wafanyakazi wa Serikali walitangaziwa na Rais wa Jamahuri ya Muungano…