Kumbe Hata Wewe Unaweza Kuikopesha Serikali na Ukatajirika?

Rafiki yangu mpendwa, Mara nyingi tunaposikia suala la deni la taifa au mikopo kwa serikali, mawazo yetu yanakimbia moja kwa moja katika nchi zilizoendelea pamoja na mashirika ya kimataifa kama vile Shirika la Fedha Duniani, Benki ya Dunia na mengine mengi. Hawa ndio wakopeshaji wakuu wa Serikali. Ndiyo, hawa ndiyo wakopeshaji wakubwa wa Serikali, lakini…

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuepuka Kazi yako Kugeuka kuwa Ibada ya Sanamu

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Je, Unaelewa nini kuhusu kuabudu sanamu? Je, Unahusika katika ibada ya sanamu? Je, Wapagani ndio waabudu sanamu tu? Watu wengi, hasa wa kizazi hiki, ni wanaabudu sanamu lakini hawajui kuwa ni waabudu sanamu. Leo nitakushirikisha namna moja tu kati ya nyingi  ambavyo unaweza kuwa unaabudu sanamu bila wewe kufahamu. Nitakushirikisha…

Hii ni aina nyingine ya Uwekezaji Ambao Mtu Wa Kisasa Kama Wewe Anapaswa Kuwa Nao

Rafiki yangu mpendwa , Katika makala yangu iliyopita nilikushirikisha  juu ya aina ya uwekezaji wa kisasa ambao mtu wa kisasa kama wewe ni muhimu kuwa nao. Aina hiyo ya Uwekezaji huo ni uwekezaji katika masoko ya dhamana. Katika makala hayo, nilikueleza kuwa uwekezaji katika masoko ya dhamana si uwekezaji mpya duniani lakini ni uwekezaji mpya…

Huu Ndio Uwekezaji ambao Mtu wa Kisasa Kama Wewe Anapaswa Kuwa Nao

Rafiki yangu Mpendwa, Kuna aina nyingi za uwekezaji ambazo watu wamekuwa wakizifanya. Baadhi ya aina hizo ni uwekezaji katika ardhi na majengo kwa kuwa na ardhi ya kukodisha na kujenga nyumba za kupangisha, kuweka fedha benki ili kupata riba, kuwekeza katika vipaji na talanta ulizo nazo kama vile utunzi na uimbaji wa nyimbo, michezo mbalimbali,…

Hizi Ndizo Sababu Kwanini Kila Mtu Anapaswa kuwa na Biashara

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Katika dunia ya leo, karibu kila mtu analalamika juu ya ugumu wa maisha. Hata wafanyakazi wenye ajira za kudumu nao ni miongoni mwa watu wanaolalmikia ugumu wa maisha.Watu wanapata pesa kila siku au kila mwezi lakini watakuambia haitoshi. Umewahi kujiuliza tatizo ni nini? Zinaweza kuwepo sababu nyingi kwa nini karibu…

Hii ndiyo tofauti kati ya kuhubiri na kufundisha

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Kabla Bwana wetu Yesu Kristo hajapaa kwenda mbinguni, alitupatia wajibu muhimu unaohusiana na kuwaandaa watu kwa ajili ya ufalme aliokuwa anaenda kutuandalia. Wajibu huo ni kuhubiri habari njema za wokovu kutoka kwa Mungu, yaani Injili na vilevile kuwafundisha watu kuyashika maelekezo yote ya Mungu. Agizo la Yesu kuhusu wajibu huu…

Hii  Ndiyo Siri ya Kuwa Mhubiri Bora

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Mojawapo ya wajibu mkuu ambao Mungu amelikabidhi kanisa ni kuhubiri Injili, yaani kueneza habari njema za wokovu. Ni agizo alilolitoa Yesu kwa wafuasi wake. “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe “(Marko 16:15). Kutokana na idadi ndogo ya wachungaji katika makanisa mengi, mahubiri mengi makanisani na yale ya…

Kwa utaratibu wa Biblia, si kila mhitaji lazima asaidiwe

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Ni wajibu wa wakrisito kuwasaidia wahitaji katika jamii. Hivyo, zaidi ya kutoa zaka na sadaka kanisani, wakristo yawapasa kutenga kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji. Suala hili ni la kibiblia maana ziaidi ya kusisitizwa katika maadniko, ipo mifano mingi katika maandiko ya watu waliotoa misaada kwa wahitaji.…

Kama Mungu ana uwezo wa kutulinda sisi na mali zetu, kwa nini tukate bima ?

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Kuna mitazamo tofauti miongoni mwa wakristo kuhusu suala la bima. Wapo wanaounga mkono kukata bima ya aina yoyote lakini wapo wengine ambao wana mtazamo kuwa kukata bima kunaonesha upungufu wa imani juu ya uweza wa Mungu. Kwa sababu ya mgawanyiko huu wa mtazamo, tutajadili kidogo suala hili. Kwanza ieleweke kuwa,…

Haya ndiyo mambo muhimu ya kuzingatia katika uwekezaji

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Watu wengi hutamani kuingia katika uwekezaji ili wawe na kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Kwa upande mwingine, kuna watu wengi ambao hawataki kuingi katika uwekezaji kwa kuogopa hatari zilizoko kwenye uwekezaji. Vilevile, kuna wawekezaji ambao huamua kuondoka kabisa katika uwekezaji na kufanya shughuli zingine baada ya kukumbana na…