Unapopiga Kura Katika Uchaguzi wa Leo, Usisahau Kujipigia Kura Wewe Mwenyewe hata Kama Hujagombea

Rafiki yangu mpendwa, Leo ni siku muhimu kwa Watanzania—Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Wananchi wanachagua viongozi wa vijiji, mitaa, na vitongoji, wakiwemo wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa. Kama viongozi mbalimbali walivyosisitiza, uchaguzi huu una umuhimu mkubwa kwa maendeleo yetu. Kwa hiyo, tunapaswa kujitokeza kwa wingi na kutumia haki yetu ya kikatiba kuwachagua viongozi … Read more

Kila Siku Unauza Kitu Bila Kujua: Huduma Mbovu kwa Wateja Wako Itakugharimu

Rafiki yangu mpendwa, Karibu tena katika somo jingine katika mfululizo wa masomo kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja ambayo tuliyaanza wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoadhimishwa duniani kote tarehe 7-13 Oktoba, 2024. Hadi sasa, tumeshajifunza mengi muhimu kuhusu umuhimu wa kuwahudumia wateja wetu kwa ubora wa hali ya juu. Katika somo hili, … Read more

Kila Siku Unauza Kitu Bila Kujua: Mara zote Fanya Kilicho Sahihi Unapouza

Rafiki yangu mpendwa, Karibu tena kwenye somo lingine la utoaji wa huduma bora kwa wateja, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa masomo tuliyoyaanza wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoadhimishwa duniani kote tarehe 7-13 Oktoba. Masomo haya ni mchango wangu katika  maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Naamini umeweza kupata maarifa muhimu yanayoweza … Read more

Kila Siku Unauza Kitu Bila Kujua: Mjue Mteja Unayemuuzia

Rafiki yangu Mpendwa,Katika wiki hii ya Huduma kwa Wateja, nakukaribisha kwenye sehemu ya pili ya mfululizo wa makala kuhusu Utoaji wa Huduma Bora kwa Wateja. Katika makala ya kwanza tulijifunza kwamba kila mmoja wetu anauza kitu katika maisha, iwe ni bidhaa, huduma, au hata maarifa. Bila shaka, ulichukua muda kutafakari kuhusu kile unachouza. Leo tunajadili … Read more

Kila Siku Unauza Kitu Bila Kujua: Gundua Unachouza

Wengi wetu tunapofikiria juu ya suala la kuuza, tunahusisha mara moja na wafanyabiashara wanaouza bidhaa na huduma mbalimbali. Hata hivyo, dhana hii imejikita katika uelewa finyu wa ukweli wa msingi kwamba kila mtu, kwa namna moja au nyingine, ni muuzaji. Uuzaji hauishii kwa wale wanaofanya biashara pekee, bali unahusu kila mtu katika hali tofauti za … Read more

Hizi Ndizo Kanuni za Matumizi ya Simu ambazo Watu Wastaarabu Huzifuata

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Katika ulimwengu wa leo uliogubikwa na teknolojia, mawasiliano ya simu ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu ya kila siku. Simu za zimekuwa zikitumika kwa kiasi kikubwa katika mawasiliano ya binafsi na ya kikazi. Hata hivyo, ni muhimu kufuata kanuni za adabu na mienendo sahihi katika matumizi ya simu ili … Read more

Waraka wa Wazi kwa Wahitimu wa Elimu ya Juu 2023- sehemu ya 4

Unaweza Kuanzia Wapi Katika Safari ya Kujiajiri? Rafiki yangu Mpendwa, Karibu tena mpenzi msomaji katika mwendelezo wa waraka kwa wahitimu wa elimu ya juu. Katika sehemu iliyopita ya waraka wangu, nilikuahidi kuwa  nitakushauri ni wapi unaweza kuanzia katika safari yako ya kujiajiri baada ya kumaliza masomo yako. Najua kabisa ya kwamba nikikuambia ujiajiri, utanijibu kuwa … Read more

Waraka wa Wazi kwa Wahitimu wa Elimu ya Juu 2023- sehemu ya tatu

Kabla hujaingia kwenye ujasiriamali soma hapa kwanza Karibu tena mpenzi msomaji katika mwendelezo wa waraka wa wazi kwa wahitimu wa elimu ya juu wa mwaka 2023. Katika makala yaliyopita ambayo ilikuwa sehemu ya pili ya waraka huu, nilikupatia mambo kadhaa unayopaswa kuyafahamu kabla hujaanza kusaka ajira. Kati ya mambo hayo, nilikushauri kufanya maamuzi ya kujiajiri … Read more

Waraka wa Wazi kwa Wahitimu wa Elimu ya Juu 2023- Sehemu ya Pili

Kabla ya Kuzunguka na Bahasha Kusaka Ajira, Nina Ujumbe Wako Rafiki yangu mpendwa, Karibu tena mpenzi msomaji katika mwendelezo wa waraka wa wazi kwa wahitimu wa elimu ya juu 2023. Katika makala yaliyopita niliwaonesha namna ambavyo mmekuwa mkidaganywa na kudanganyana kuhusu maisha baada ya masomo yenu hususani kuhusu upatikananji wa ajira na mishahara mizuri. Ukweli … Read more