Kama Mungu ana uwezo wa kutulinda sisi na mali zetu, kwa nini tukate bima ?

Kama Mungu ana uwezo wa kutulinda sisi na mali zetu, kwa nini tukate bima ?

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Kuna mitazamo tofauti miongoni mwa wakristo kuhusu suala la bima. Wapo wanaounga mkono kukata bima ya aina yoyote lakini wapo wengine ambao wana mtazamo kuwa kukata bima kunaonesha upungufu wa imani juu ya uweza wa Mungu. Kwa sababu ya mgawanyiko huu wa mtazamo, tutajadili kidogo suala hili. Kwanza ieleweke kuwa,…

Fedha yako inaweza kuimarisha au kubomoa Ndoa yako

Fedha yako inaweza kuimarisha au kubomoa Ndoa yako

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Tafiti zilizofanyika katika nchi mbalimbali zinaonesha kuwa mojawapo ya mambo yanayooongoza kusababisha migogoro na kuvunjika kwa ndoa ni fedha. Kwa mfano, Mwaka 2017, kampuni moja ya kimarekani inayojishughulisha na utafiti na utoaji wa elimu ya masuala ya fedha itwayo Ramsey solutions, ilifanya utafiti uliowahusisha watu 1072 nchini humo. Lengo la…

Haya ndiyo mambo muhimu ya kuzingatia katika uwekezaji

Haya ndiyo mambo muhimu ya kuzingatia katika uwekezaji

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Watu wengi hutamani kuingia katika uwekezaji ili wawe na kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Kwa upande mwingine, kuna watu wengi ambao hawataki kuingi katika uwekezaji kwa kuogopa hatari zilizoko kwenye uwekezaji. Vilevile, kuna wawekezaji ambao huamua kuondoka kabisa katika uwekezaji na kufanya shughuli zingine baada ya kukumbana na…

Hizi Ndizo Kanuni Za Kufanya Biashara Kwa Mkristo

Ndugu yangu mpendwa katika Kristo, Hakuna ubishi kwamba biashara ni njia mojawapo ya uhakika ya kujipatia kipato kisicho na kikomo. Hivyo, ni vema kila mmoja anayetamani kufanikiwa kifedha awe na biashara hata kama na vyanzo vingine vya kipato. Kama utaamua kufanya biashara, yakupasa ujue kuwa biashara ina kanuni zake. Zipo kanuni za jumla ambazo mfanyabiashara…

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kufundisha na Kuhubiri Kwa Watoto wa Siku Hizi

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kufundisha na Kuhubiri Kwa Watoto wa Siku Hizi

Rafiki yangu mpendwa katika Krsito, Tunaishi katika karne ambayo imepewa jina la “Karne ya Sayansi na Teknolojia”. Maendeleo makubwa ya Sayansi na teknolojia yamesababisha mabadiliko karibu katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu na mabadiliko hayo yanatokea kwa kasi sana kuliko karne zilizopita. Maendeleo tunayoyashuhudia si kitu cha kushangaza kwa wasomaji wa Biblia maana ni…

Unajua Umuhimu wa kuwafundisha watoto elimu ya kiroho?

Unajua Umuhimu wa kuwafundisha watoto elimu ya kiroho?

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wana wasiwasi kuhusu kuwalea watoto katika ulimwengu wa leo unaokabiliwa na changamoto za utandawazi. Hata hivyo, hatuna sababu ya kuwa na wasiwasi kama tukifuata ushauri huu: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee”(Mithali 22:6). Watoto waendeleapo kukua, wanahitaji ‘njia’, yaani kanuni…

Utashangaa Kusikia Siri hii Kutoka Kwa Wasomaji wa Vitabu

Utashangaa Kusikia Siri hii Kutoka Kwa Wasomaji wa Vitabu

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo,  Umewahi kusikia kuhusu jarida la Forbes? Hili ni jarida maarufu la kibiashara la Marekani ambalo huchapisha masuala ya fedha, viwanda, uwekezaji na masoko. Jarida hili ni maarufu sana duniani kwa kutoa takwimu, orodha na madaraja ya vitu kama vile orodha ya watu matajiri (mabilionea) zaidi duniani (the Word’s Billionaires). Januari…

Hiki Ndicho Mungu Aliagiza Tufanye Kabla Ya ‘Kula Bata’

Hiki Ndicho Mungu Aliagiza Tufanye Kabla Ya ‘Kula Bata’

Rafiki yangu mpendwa, Katika makala yangu iliyopita, nilieleza vile namna ambavyo Mungu aliagiza “tule bata”. Katika makala hiyo nilieleza kuwa kula bata kunatafsiriwa kama kupumzika na kufurahia maisha. Kupitia biblia, Mungu ameelekeza tuwe na muda kupumzika vya kutosha kila siku na siku moja kwa kila juma. Leo nitakushirikisha kitu muhimu cha kuzingatia kabla ya “kula…

Hivi Ndivyo Mungu Alivyoagiza ‘Tule Bata’.

Hivi Ndivyo Mungu Alivyoagiza ‘Tule Bata’.

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo, Msemo “kula bata” umekuwa maarufu sana katika siku za hivi karibuni ukiwa unatumiwa zaidi na vijana. Msemo huu unatumika kumaanisha kufurahia maisha. Japo kila mtu anatafsiri yake kuhusu kufurahia maisha, mara nyingi “kula bata” ni kufurahisha maisha kunakohusisha kutumia pesa katika mambo mbalimbali kama vile burudani, kula  na kunywa vitu…