KITABU: MWONEKANO WA MKRISTO

MWONEKANO WA MKRISTO: KANUNI ZINAZOKUBALIKA KIBIBLIA, KIAFYA NA KIJAMII KUHUSU MAVAZI, MAPAMBO NA VIPODOZI

Kitabu hiki kimechambua mafundisho ya Biblia kutoka Agano la kale na Agano jipya ili kupata kanuni za kibiblia kuhusiana na mavazi, mapambo na vipodozi na namna kanuni hizo zinavyoweza kutumika katika jamii ya leo. Vilevile, kuna uchambuzi wa kihistoria kuhusiana na mitazamo na mienendo ya Wakristo kuhusiana na mwonekano wa nje katika vipindi mbalimbali vya historia ya kanisa katika madhehebu mbalimbali ya Kikristo.

Kitabu hiki kimesheheni taarifa na maelezo ya kitaalamu kuhusu athari za kiafya za mavazi, mapambo na vipodozi kutoka katika vyanzo vinavyoaminika hususani vitabu, machapisho na matokeo ya tafiti mbalimbali kutoka mamlaka zinazotambuliwa na pia kutoka kwa wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali za taaluma ya afya.

Kitabu hiki ni kwa ajili ya watu wote wanaohitaji kupata uelewa sahihi kuhusu mwonekano wa Mkristo katika mavazi, mapambo na vipodozi kwa kutoa kanuni za kibiblia na namna zinavyoweza kutumika katika jamii ya leo. Lengo la kitabu hiki ni kuwasaidia Wakristo kuamua wavae nini, wajipambeje na watumie vipodozi vya aina gani kwa kuongozwa na kanuni za kibiblia, kiafya na maadili ya jamii yao badala ya kuongozwa na mitazamo yao na ya watu wengine ambayo baadhi yake si sahihi.

Kwa kusoma kitabu hiki, utapata maarifa juu ya mambo yafuatayo:

Kwanza, Umuhimu wa mwonekano mzuri wa nje kwa Mkristo

Pili, Mavazi, Mapambo na vipodozi katika Agano la Kale

Tatu, Mavazi, Mapambo na vipodozi katika Agano jipya

Nne, Je ni sahihi kwa Mkristo kuvaa pete ya Uchumba au Ndoa? 

Tano, Utajuaje kuwa aina fulani ya kipodozi ni salama kwa afya?

Sita, Hatari za kiafya na kiroho za urembo bandia kama vile nywele bandia (rasta, wig, weaving), kunenepesha makalio, mapaja, nyonga na matiti, kope za bandia, kucha za bandia  

Saba,  Uvaaji wa viatu kwa afya na mwonekano bora

Nane, Mkristo ambaye ni mtumishi wa umma anapaswa kuwa na mwonekano gani?

Tisa, Siri na kanuni zinazoweza kukufanya upendeze kwa chochote utakachovaa

Kumi, Uvaaji wa tai na kanuni zake.

Namna ya kitabu kitabu hiki

Ili uweze kuelekezwa namna ya kupata kitabu hiki, wasiliana nasi kupitia namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (Devotha Shimbe) na E-mail: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com